SIMBA NDANI YA DAR KAMILI KWA KETE YA MWISHO

NYOTA wa Simbaa baada ya kumaliza kete yao ya 29 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC wamerejea Dar kwa maandalizi ya kete ya mwisho msimu wa 2023/24.

Ni Mei 25 ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya dakika 90 ulisoma Simba 1-0 KMC.

Bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza dakika ya tatu ya mchezo kutokana na makosa ya mlinda mlango wa KMC.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 66 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo sawa na Azam FC kwa pointi iliyo nafasi ya pili tofauti kwenye mabao ya kufunga na kufungwa.

Mei 26 2024 kikosi cha Simba kimerejea Dar kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa funga msimu wa 2023/24 unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 28.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ikiwa ugenini Simba ilikomba pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 lilifungwa na Clatous Chama.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wao ujao watafanya kazi kubwa kupata pointi tatu.

“Tunatambua umuhimu wa mchezo wetu ujao hivyo tutapambana kupata pointi tatu muhimu, mashabiki wajitokeze kwa wingi.”