YANGA WANABALAA ZITO

YANGA vinara wa Ligi Kuu Bara wana balaa zito kutokana na kasi yao kuwa kwenye ubora kwenye mechi ambazo wanacheza msimu wa 2023/24.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa msimu wa 2023/24 walitwaa taji hilo baada ya kufikisha pointi 71 mchezo wao wa 27 dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Manungu.

Kwenye mchezo wa 28 walipata ushindi dhidi ya Dodoma Jiji kwa kukomba pointi tatu ushindi wa mabao 4-0 ambapo kwenye mchezo huo Aziz KI alifunga mabao mawili nakufikisha mabao 17 akiwa namba moja kwenye msimamo.

Ki ameweka wazi kuwa ushindi kwao ni jambo la msingi na kufikisha mabao 17 haimpi presha yakufikiria tuzo ya ufungaji bora.

“Ninafurahi kuona kwamba tunapata ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza muhimu nikuona kwamba kila mchezaji anafurahia kile ambacho kinapatikana uwanjani kwa kupata ushindi.

“Kikubwa ni matokeo kuhusu tuzo ya ufungaji bora hilo sifikirii kwa kuwa bado kuna mechi tunacheza na kila mchezaji anafanya vizuri.”

Mabao 17 kibindoni anakuwa namba moja akimuacha Feisal Salum wa Azam FC mwenye mabao 16.