SIMBA KWENYE HESABU NDEFU

WAKIWA na mchezo dhidi ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Arusha Mei 25 2024 benchi la ufundi la timu hiyo limebainisha kuwa hesabu ni kupata matokeo kwenye mechi ambazo wanacheza.

Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba ushindi wake mkubwa akiwa na timu hiyo ilikuwa mchezo dhidi ya Geita Gold walipopata ushindi wa mabao 4-1 baada ya dakika 90 kukamilika.

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 63 baada ya kucheza mechi 28 sawa na Azam FC iliyo nafasi ya pili tofauti kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Mgunda amesema: “Mapema kabisa tulipoteza katika mchezo wetu uliopita tulipoanza tukafungwa lakini tunamshukuru Mungu katika mchezo wetu tulitoka nyuma tukiwa tumefungwa bao moja na kufunga mabao manne.

“Kilichotokea ni kuona kwamba tuna kazi ya kupata nafasi na kuzitumia katika kila mchezo ambao tunacheza kutokana na ushindani ambao upo kwa kuwa kila mchezaji anatambua tuna kazi muhimu.

“Vijana kwenye mechi ambazo tumecheza tunaona kwamba kazi kubwa katika mechi zetu hasa katika kutumia nafasi ambazo tunazipata kutokana na kushindwa kuwa katika kupata matokeo kwani kikubwa initia moyo kwenye mechi ambazo tunacheza.

“Wachezaji wetu wanacheza na kujituma kwa kuwa tuna mechi nyingine ambazo zipo katika mechi ambazo tunacheza bado tuna kazi ya kufanya katika mechi zijazo.”