MWAMBA NTIBANZOKIZA KAIBUKA

MWAMBA Saido Ntibanzokiza anafikisha mabao 9 ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold.

Mei 22 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Simba 4-1 Geita Gold ambapo pointi tatu mazima zilibaki Msimbazi.

Ni Geofrey Julius alianza kumtungua Hussen Abel kipa wa Simba dakika ya 11 na dakika ya 45 bao la kusawazisha kwa Simba lilipatikana kupitia kwa Ntibanzokiza baada ya Shomari Kapombe kuchezewa faulo ndani ya 18.

Alirejea kambani kwa mara nyingine dakika ya 72 kwa pigo la faulo iliyosababishwa na Willy Onana aliyeingia kipindi cha pili alitokea benchi.

Ladack Chasambi alipachika mabao mawili ilikuwa dakika ya 86 na 90+3 kwenye mchezo huo ambao Geita Gold walishuhudia nyota wao Samuel Onditi akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 63 ikiwa nafasi ya tatu safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 56 sawa na ile ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Yusuph Dabo.

Ikumbukwe kwamba mwamba huyo aliibuka ndani ya Simba akitokea Geita Gold.