FEI TOTO KAZIDISHA KASI HUKO

WAKATI Azam FC inakomba pointi tatu mazima dhidi ya JKT Tanzania mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Meja Isamuhyo mwamba Feisal Salum kiungo mshambuliaji wa Azam FC aligusa mpira mara 39.

Katika dakika 90 alizokomba na kushuhudia ubao ukisoma JKT Tanzania 0-2 Azam FC, Mei 21 2024 alipiga mashuti matatu ambayo yalilenga lango na katika hayo moja lilizama nyavuni akitumia mguu wake wa kulia.

Nyota huyo mzawa alikokota mpira mara nne na miguso ndani ya box mara tano kwa mujibu ya twakwimu za Ligi Kuu Bara.

Fei alipachika bao lake la 16 dakika ya 90+4 na bao la kwanza lilipachikwa na Abdul Sopu dakika ya 30 kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kubaki namba mbili na pointi 63 baada ya kucheza jumla ya mechi 28 wapo sawa na Simba iliyo nafasi ya tatu tofauti kwenye mabao ya kufungwa.

Azam FC imefungwa mabao 20 huku ukuta wa Simba ukiwa umeruhusu kufungwa mabao 25 kwenye mechi 28.

Fei anafikisha mabao 16 akiwa namba moja kwa vinara wa utupiaji Bongo huku akiwa katoa jumla ya pasi 7 za mabao msimu wa 2023/24.