FAINALI YA YANGA V AZAM KUPIGWA ZANZIBAR

RASMI Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kwamba fainali ya CRDB Federation Cup inatarajiwa kuchezwa Zanzibar.

Ni Uwanja wa New Amaan Complex unatarajiwa kutumika kwenye fainali ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi watakabiriana na Azam FC ambapo kwenye fainali iliyopita walicheza na Azam FC na Yanga ikatwaa ubingwa kwa ushindi wa bao 1-0.

Awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Babati mkoani Manyara lakini kwa sasa ngoma imetangazwa itakuwa ni Zanzibar.

Mechi hiyo inayozikutanisha Azam FC dhidi ya Yanga SC, itachezwa Juni 2, 2024 saa 2:15 usiku