DODOMA JIJI YAPIGWA 4G NA YANGA

MASTA Aziz KI kiungo mshambuliaji wa Yanga amepindua Meza ya vita ya ufungaji bora baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Dodoma Jiji na kufikisha mabao 17 akiwa namba moja chati ya ufungaji.

KI amefunga mabao mawili wakati ubao wa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ukisoma Dodoma Jiji 0-4 Yanga ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.

Dakika ya 10 Clement Mzize alianza kufunga bao la kuongoza, KI alipachika bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 45+4 ni yeye mwenyewe aliisababisha.

Kipindi cha pili Maxi Nzengeli alipachika bao la nne dakika ya 78 ikiwa ni baada ya kushuhudia baoa 17 la KI alilofunga dakika ya 50 akitumia pasi ya Mzize.

Yanga imekomba pointi tatu na imebakiwa na mechi mbili baada ya mchezo wa leo wakishinda 4 G wakifikisha pointi 74 kibindoni ndani ya msimu wa 2023/24.