YANGA KUJA NA SHEREHE KUBWA YA UBINGWA

MABINGWA mara 30 wa Ligi Kuu Bara wamebainisha kuwa wanakuja na mpango kazi mkubwa wa sherehe za ubingwa wa ligi kwa msimu wa 2023/24.

Ipo wazi kuwa Yanga baada ya kucheza mechi 27 ikibakiwa na mechi tatu imetwaa taji la ligi chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi.

Kwa sasa Yanga ipo Arusha kuelekea kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wa CRDB Federation Cup hatua ya nusu fainali dhidi ya Ihefu unaotarajiwa kuchezwa Mei 19 2024.

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga ameweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kufanya sherehe kubwa ya ubingwa yenye hadhi ya dunia.

“Baada ya kukamilisha mpango kazi wa kutwaa ubingwa sasa ni muda wakusubiri ratiba nzima itakavyokuwa kwenye upande wa sherehe za ubingwa na safari hii itakuwa ni level za dunia.

“Ambacho bingwa unatakiwa kukifanya kwa sasa ni kuchukua jezi ya ubingwa ipo tayari makao makuuu ya Yanga kisha hapo utakuwa tayari umeshakamilisha kazi ya kwanza kuwa miongoni mwa wale watakaokuwa kwenye sherehe hizo ambapo tutatangaza itakuwa ni lini na mchezo upi.”.

Habari zinaeleza kuwa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons umechaguliwa kuwa mchezo maalumu wa kutangazia ubingwa ambapo unaweza kuchezwa nje ya Dar badala ya Uwanja wa Azam Complex.