Home Sports YANGA; 5G KWA SIMBA HAIKWEPEKI

YANGA; 5G KWA SIMBA HAIKWEPEKI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kichapo cha mabao 5 mbele ya Simba hakikimbiliki kwa namna yoyote kwa kuwa kila hesabu watakazofanya inakuja 5.

Ipo wazi kuwa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga na mchezo wa mzunguko wa pili ilikuwa Yanga 2-1 Simba.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa kikubwa ambacho kipo ni ushindi wa mabao 5 kwenye mechi zao zote.

“Ambacho kipo kwa sasa kitaalamu hauwezi kukwepa 5 kwa watani zetu wa jadi Simba wakichukua mabao matano tuliyofunga mzunguko wa kwanza kisha wakaongeza na mawili inakuwa 7-2.

“Ukitoa mabao mawili inabaki 5, hivyo mabao matano hayakwepeki kwa namna yoyote tumewaachia wasumbuke nayo hayo,”.

Previous articleWAKALI WAKUCHEKA NA NYAVU HAWA HAPA
Next articleSIMBA NA AZAM KUSHIRIKI KOMBE LA MUUNGANO