Home Sports HUU HAPA MTAMBO WA MABAO SIMBA

HUU HAPA MTAMBO WA MABAO SIMBA

NDANI ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha kuna mitambo mingi ya mabao lakini kwa sasa namba moja ni Clatous Chama.

Ipo wazi kwamba kasi ya Chama msimu wa 2023/24 imeporomoka licha yakuwa na uhakika kikosi cha kwanza kuna sababu nyingi zinasababisha yote hayo ikiwa ni pamoja na wachezaji wa Simba kuongoza kwenye kutotumia nafasi ambazo wanatengeneza.

Ikumbukwe kwamba wakati timu hiyo ikiambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ihefu Uwanja wa Liti nafasi zaidi ya tano zilitengenezwa lakini hazikutumiwa na wachezaji wa Simba kwenye safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Michael Fred.

Chama amehusika katika mabao 12 kati ya 40 yaliyofungwa na timu hiyo iliyonafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 20.

Ni mabao sita kafunga na kutoa pasi sita za mabao kituo kinachofuata ni mchezo wa ligi dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa, Aprli 20 2024.

Previous articleREAL MADRID, BAYERN MUNICH WATINGA NUSU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA, MAN CITY & ARSENAL ‘OUT’
Next articleAZAM FC WABANANA NA MASHUJAA