Home Sports SIMBA KAMILI GADO KUELEKEA ZANZIBAR KWA MAANDALIZI YA DABI

SIMBA KAMILI GADO KUELEKEA ZANZIBAR KWA MAANDALIZI YA DABI

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa upo tayari kwa maandalizi ya mechi zake zote ziazofuata ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Aprili 20 2024 ambapo Simba itakaribishwa na vinara wa ligi Yanga wenye pointi 55 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 46.

Ipo wazi kuwa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 hivyo mchezo ujao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, Simba wakihitaji kulipa kisasi na Yanga kuendeleza rekodi ya ushindi.

Kikosi cha Simba leo Aprili 16 kinatarajiwa kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kambi maalumu kwa maandalizi ya mechi zilizobaki.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema: “Tupo tayari kwa maandalizi ya mechi zetu zote na Mungu akipenda Jumanne ya Aprili 16 tutaelekea Zanzibar kwa kambi maalumu kwa mechi zetu ambazo zimebaki,”.

Previous articleCheza Kasino ya 40 Lucky Sevens Ushindi ni Kupitia Matunda
Next articleHAWA WAKALI KWENYE KUFUNGA NA KUTOA PASI, MSHAMBULIAJI MMOJA