Home Sports SIMBA YAANDIKA REKODI HII TATU BORA

SIMBA YAANDIKA REKODI HII TATU BORA

KLABU ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha imeandika rekodi yake ndani ya tatu bora kwa kuwa timu iliyoruhusu mabao mengi yakufungwa.

Ipo wazi kuwa Simba inatarajiwa kutupa kete yake nyingine leo Aprili 13 dhidi ya Ihefu mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti, Singida.

Wachezaji wa Simba wanaonekana kutokuwa imara kwenye ukabaji ndani ya mechi za ushindani jambo linalowafanya waingie kwenye orodha ya timu iliyofungwa mabao mengi ndani ya ligi.

Ni mabao 18 imefungwa baada ya kucheza jumla ya mechi 19 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo na namba moja kwa timu ambazo zipo ndani ya tatu bora kufungwa mabao mengi.

Timu ya Yanga ni namba moja kwa timu iliyofungwa mabao machache ambayo ni 11 baada ya kucheza mechi 20 na Azam FC ni namba mbili ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 21 imefungwa mabao 16.

Previous articleCHEKI RATIBA YA LIGI LEO
Next articleCheza Kasino Bulls Eye Bells Ushinde Bonasi na Jackpot Kubw