Home Sports SPORTPESA DABI MLANGONI, RATIBA HII HAPA

SPORTPESA DABI MLANGONI, RATIBA HII HAPA

KAZI bado inaendelea ndani ya uwanja kwa kila timu kusaka pointi tatu baada ya dakika 90.

Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa ni mzunguko wa pili unaendelea kwa kila timu kupambania kufikia malengo ya kupata pointi tatu.

Ijumaa ya Aprili 12 kuna mechi ambazo zinatarajiwa kuchezwa ni Tanzania Prisons v KMC huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine.

Mashujaa ya mwisho wa reli Kigoma wao itakuwa dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambapo mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika.

Aprili 13 2024 itakuwa ni Geita Gold v Mtibwa Sugar, Ihefu dhidi ya Simba, Uwanja wa Liti, Tabora United dhidi ya JKT Tanzania, Kagera Sugar dhidi ya Dodoma Jiji.

Hii hapa Sportpesa Dabi

Aprili 14 2024 Singida Fountan Gate inayodhamiwa na SportPesa itakuwa na kazi dhidi ya Yanga inayodhamiwa pia na SportPesa..

Mbali na SportPesa Dabi pia Namungo FC itawakaribisha Azam FC katika mchezo wa mzunguko wa pili.

Previous articleDIAMOND AMETAJA MAMBO MUHIMU YA BOSS, SIO WA MCHEZOMCHEZO
Next articleBOSI SIMBA: MATOKEO YANAUMIZA KWELIKWELI