Home Uncategorized SIMBA: TUMEUMIZWA VIBAYA MNO

SIMBA: TUMEUMIZWA VIBAYA MNO

UONGOZI wa Simba umebainisha kwamba umeumizwa vibaya kukwama kupata matokeo kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika.

Ilikuwa ni kwenye CRDB Federation raundi ya nne ambapo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mashujaa 1-1 Simba na kwenye penalti ilikuwa Mashujaa 6-5 Simba.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua namna mwendo ulivyo matokeo amabayo wameyapata hayajawafurahisha.

“Tumesikitishwa vibaya mno na matokeo ambayo tumeyapata kwa kuwa sio matokeo mazuri lakini ni mpira na hayo yametokea ambacho tunakifanya ni kupambana kurejea kwenye ubora.

“Wachezaji wanakazi kubwa yakufanya kwenye mechi zetu zinazofuata na tunaamini kwamba itakuwa hivyo,mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

Previous articleKasino Mtandaoni Yenye Njia Nyingi za Ushindi|81 Crystal Fruits
Next articleCHOMOKA NA BAJAJI CHEZA SUPER HELI MCHEZO MPYA WA KASINO