Home Sports SIMBA YASIKITIKIA MATOKEO YAKE

SIMBA YASIKITIKIA MATOKEO YAKE

UONGOZI wa Simba umeyasikitikia matokeo yake inayopata ndani ya uwanja katika mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.

Ipo wazi kuwa mwendo wa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika umegotea hatua ya robo fainali na kwenye CRDB Federation Cup wamegotea raundi ya nne.

Aprili 9 2024 ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ulisoma Mashujaa 1-1 Simba ndani ya dakika 90 na mshindi alipatikana kwa penalti ilikuwa Mashujaa 6-5 Simba.

Ahmed Ally, Meneja Idara Habari na Mawasiliano Simba amebainisha kuwa wamepata matokeo ambayo hayajawafurahisha jambo ambalo linawapa masikitiko.

“Hatujapata matokeo mazuri kwenye mechi zetu za hivi karibuni tunasikitika vibaya, matoeo yametuumiza vibayavibaya kweli hivyo tunaamini kwamba tuna muda wa kufanyia kazi makosa yetu,”.

Previous articleYANGA YAINGIA MCHECHETO KUWAKABILI DODOMA JIJI
Next articleM-BET YAMZAWADIA MSHINDI WA PERFECT 12 MILIONI 140.5