UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa moto wao kwenye anga la kimataifa hautazima kwa kuwa wapo imara kwenye kupambania nembo ya Yanga na Tanzania kiujumla. Ikumbukwekwamba katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga imegotea hatua ya robo fainali ilipopoteza kwa penalti 3-2 dhidi ya Mamelodi Sundowns.