Home Uncategorized MITAMBO YA KAZI YANGA IPO KAMILI KIMATAIFA

MITAMBO YA KAZI YANGA IPO KAMILI KIMATAIFA

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga leo watakuwa Uwanja wa Mkapakusaka ushindi dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Kwenye mchezo wa leo mitambo ya kazi ambayo haikuwa fiti inatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi miongoni mwao ni Khalid Aucho, Pacome, Zawad Mauya huku YaoYao na Kibwana Shomari ripoti ya daktari itaamua uwepo wao.

Mastaa wa Yanga ambao walikuwa hawajaripoti kambini ikiwa ni Aziz KI na Diarra wapo kambini kamili kwa mchezo huo.

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kupambana kupata ushindi.

“Tunatambua kwamba mchezo wetu dhidi ya Mamelod Sundowns utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya kupata ushindi ndani ya dakika 90 inawezekana na muda ni sasa,”.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa tatu usiku Uwanja wa Mkapa ikiwa ni robo fainali ya kwanza na ile ya pili itakuwa nchini Afrika Kusini.

Previous articleAZIZ KI WA YANGA ANA BALAA HUYO
Next articleVIDEO: YANGA: WANAPOTUKATIA TAMAA HAPO TUNAPATAKA, TUTAWAONYESHA