Home Sports TWIGA STARS KAZINI LEO, HAKUNA KIINGILIO

TWIGA STARS KAZINI LEO, HAKUNA KIINGILIO

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, Bakari Shime amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu ya Afrika Kusini.

Shime ameweka wazi kuwa muda wa maandalizi waliopata walitumia kufanyia kazi makosa na kupeana mbinu ambazo zitakuwa kielelezo kwenye mchezo ndani ya dakika 90.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Februari 23 ni maalumu kwa ajili ya kufuzu Olimpiki unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar  saa 10 jioni.

Katika mchezo wa leo hakutakuwa na kiingilio hivyo ni fursa kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuishangilia timu ya taifa ya Tanzania.

Shime amebainisha kwamba wanatambua umuhimu wa mchezo wa leo na wataingia kwa tahadhari huku wachezaji wakiwa tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja.

“Wachezaji wapo tayari na maandalizi yamekamilika ambacho tunasubiri ni muda na kuona namna gani tunapata matokeo kwenye mchezo wetu muhimu ambao tunahitaji matokeo.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia mchezo wetu ambao kila timu inahitaji ushindi ndani ya uwanja. Tunaamini kwamba uwepo wao utaongeza ari kwa upambanaji ndani ya uwanja,”.

Previous articlePATA MGAO WA BIL 2 KUTOKA MERIDIANBET KASINO UKICHEZA MICHEZO YA PRAGMATIC PLAY!!
Next articleLIGI YA MABINGWA AFRIKA WABABE KAZINI