Home Uncategorized YANGA HESABU ZAO NI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

YANGA HESABU ZAO NI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa mpago mkubwa ni kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na wanaamini watafanya vizuri kwenye mechi zao.

Mchezo ujao kwa Yanga katika anga la kimataifa ikiwa hatua ya makundi ni dhidi ya CR Belouzidad unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Timu zote mbili zina pointi tano kibindoni hivyo mshindi ataongeza nafasi ya kufikia malengo ya kutinga hata ya robo fainali.

Ali Kamwe Ofisa Habari wa Yanga amesema:” Kundi la kiume ambalo tupo na  nafasi bado iko wazi kwa kila timu. Sisi Yanga fainali yetu ni Uwanja wa Mkapa Vs Belouzidad.

“Mchezo huo utakuwa ni 24/2/2024. Mpango wetu ni robo fainali. Na tutautimiza mpango huu kama tutaungana pamoja na kwenda Uwanjani kuwapa nguvu wachezaji wetu siku hiyo.

“Uwanja kujaa ndio silaha yetu ya kwanza ya kumpunguza makali Mwarabu, mashabiki tujitokeze kwa wingi muda ni sasa,”.

Previous articleCLATOUS CHAMA WA SIMBA V PACOME WA YANGA NI VITA
Next articleCheza na Ushinde kwa Kadi Kasino ya Poker Teen Patti Ndani ya Meridianbet