YANGA HAWANA JAMBO DOGO WAWAPIGIA HESABU WAARABU

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga utakuwa ni maalumu kwa ajili ya kusaka ushindi ukipewa jina la Pacome day Kitaalamu zaid.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua umuhimu wa kupata matokeo kwenye mchezo wao ujao hivyo watafanya kazi kubwa kupata ushindi.

Ipo wazi kwamba katika mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini, Yanga ilipoteza pointi tatu kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi kwa kufungwa mabao matatu.

Kamwe amesema:”Kilichosaidia CR Belouizdad ni wingi wa mashabiki wao, ukweli ni kwamba sisi sio wanyonge kimsingi hatuwezi kufanikiwa bila uwepo wa mashabiki wetu ambao kwa dakika zote tuwe na sapoti kubwa, kuanzia dakika ya kwanza mpaka dakika ya mwisho, tusishangilie matokeo tunapaswa kushangilia kila dakika kuhakikisha mwarabu anapagawa.

“Jumamosi sio mchezo wa kitoto, ni mechi ya kikubwa kweli. Benchi la ufundi kimsingi limejiandaa vya kutosha kwa upande wa mashabiki tunapaswa kufika na hasira ya kweli kila anayeamini analo jambo ambalo linaweza kusaidia timu yako kushinda basi lifanye.

“Ruksa popote ulipo usimuogope mtu wewe fanya. Hakuna masihara mchezo ujao, tukitoka sare basi ujue tumeisha. Ni siku ya Pacome Day Kitaalamu zaidi kila kitu kitakuwa hivyo, mashabiki tujitokeze kwawingi,”.