Home Sports TANZANIA PRISONS KUWAKABILI YANGA

TANZANIA PRISONS KUWAKABILI YANGA

TANZANIA Prisons inayotumia Uwanja wa Sokoine kwa mechi za nyumbani le Februari 11 inatarajiwa kuwa na kazi ya kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.

Kocha wa Prisons, Ahmad Ally ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kwa ajili ya kupambania pointi tatu.

“Ni mchezo mgumu na utakuwa na ushindani tupo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu,”.

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua kazi itakuwa kubwa kutafuta pointi tatu.

“Tunahitaji pointi tatu kwenye mchezo wetu na tunawaheshimu wapinzani wetu,”.

Previous articleMWAMBA WA LUSAKA CHAMA NA TAMKO HILI HAPA
Next articleYANGA WAMEWAACHA MBALI SIMBA