COSMOPOLITAN WAZITAKA POINTI TATU ZA PAN AFRICANS

UONGOZI wa Cosmopolitan umebainisha kuwa mpango mkubwa ni kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa Championship dhidi ya wapinzani wao Pan Africans wakiwa ugenini.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Februari 3 Uwanja wa Mabatini, Pwani kwa wababe hawa wawili kusaka pointi nani ya dakika 90.

Ikumbukwe kwamba Ofisa Habari wa Cosmopolitan, Leen Essau aliibuka ndani ya timu hiyo akitokea Pan Africans hivyo mbali na ndani ya uwanja kuwa na vita ya msako wa ushindi nje ya uwanja viongozi wanatambua kwa uzuri.

 Leen amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wapo tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

“Ni mzunguko wa pili kwetu kwa kuwa wanakumbuka mchezo wa kwanza tukiwa nyumbani tulishinda bao 1-0 na sasa tunawafuata ugenini kupata pointi tatu muhimu mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani, “ alisema Leen.

Cosmopolitan ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 18 inakutana na Pan Africans iliyo nafasi ya 14 na pointi 15.