>

SIMBA QUEENS/JKT QUEENS ZAPETA LIGI YA WANAWAKE

WASHINDANI wawili ndani ya Ligi ya Wanawake Tanzania kila mmoja kwa wakati wakati kapeta kwa kukomba pointi tatu uwanjani.

Ni JKT Queens 6-0 Baobab Queens mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.

Amina Bilal, Jackline, Donisia Minja na Stumai Abdallah huyu katupia hat trick.

Kwenye mchezo mwingine ambao ulikuwa unafuatiliwa kwa ukaribu ilikuwa ni ule uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ubao umesoma Fountain Gate 0-4 Simba Queens

Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Asha Djafar dakika ya 12, 56, Super Jentrix dakika ya 72 na Mnunkana dakika ya 84.

Vita ya ubingwa inazidi kupamba moto kila dakika kwa wababe hawa wawili ambapo JKT Queens hawa ni mabingwa watetezi.

JKT Queens ushindi wao ni kwenye mechi zote  7 wakikusanya pointi 21 Simba Queens mechi 7 pointi 19