LIGI Kuu Tanzania Bara inarejea ambapo timu zote zipo kwenye hesabu za msako wa pointi tatu muhimu.
Januari 31 Simba ilifunga kwa mchezo wa Azam Sports Federation dhidi ya Tembo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Februari Mosi Kikosi cha Simba SC, kimetua mkoani Kigoma kwa ajili ya kukabiliana na Mashujaa FC kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Februari 3, 2024 Uwanja wa Lake Tanganyika.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani na kuwapa burudani mashabiki.
“Tupo tayari kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki tunatambua ushindani ni mkubwa tupo tayari kwa ajili ya kufanya vizuri na kupata pointi tatu,”.