KHALID AUCHO AMEONGEZEWA DOZI YANGA

KIUNGO wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga, Khalid Aucho ameongezewa dozi na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ikiwa ni malengo ya kumuongezea uimara wake sambamba na mshambuliaji, Clement Mzize.

Gamondi anaendelea kuwapa mbinu wachezaji wa Yanga kwa ajili ya mechi za kitaifa na kimataifa baada ya kupishana na Kombe la Mapinduzi 2024, huku nyota wengine wakiwa katika majukumu kwenye timu zao za taifa.

 Gamondi amesema kuwa wachezaji wake wote ni muhimu kuwa fiti kwa ajili ya kuwa kwenye mwendo bora ndani ya timu katika mashindano ambayo wanashiriki.

 “Kila mmoja anatambua umuhimu wa kufanya kazi kwa umakini na kutimiza majukumu ambayo yapo na inawezekana kuwa katika ubora kwenye mechi ambazo tunacheza kwani hilo linawezekana.

“Muda uliopo ni wachezaji kuwa tayari kwa ajili ya mazoezi iwe ni Aucho, (Khalid), Maxi, (Nzengeli) wote ni muhimu kuwa makini kwenye kutimiza majukumu yao,” alisema Gamondi.

Timu hiyo kwenye ligi ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 11 ilishinda 10 na kupoteza mchezo mmoja.