Home Sports IHEFU WAPO KAMILI GADO

IHEFU WAPO KAMILI GADO

KUTOKA Mbeya ulipo Uwanja wa Sokoine kwa majirani zao Mbeya City na Tanzania Prisons amba hutumia kwa mechi za nyumbani wao wapo Mbarali ambapo hutumia Uwanja wa Highland Estate kwa mechi za nyumbani.

Hawa ni Ihefu wapo kamili gado kuelekea mechi zijazo za ushindani ili kupata matokeo mazuri kutokana na kutokuwa na mwendo mzuri kabla ya ligi kusimama.

Kocha Mkuu wa Ihefu, Mecky Mexime amesema kuwa wanaamini watatumia kwa umakini kufanya maandalizi kwa muda huu uliopo ambapo kikosi kipo Arusha.

Mexime alikuwa anakifundisha kikosi cha Kagera Sugar alitambulishwa ndani ya Ihefu hivi karibuni kwa ajili ya kukifundisha kikosi hicho.

“Ushindani ni mkubwa kwenye ligi hivyo ambacho tunakifanya kwa sasa ni maandalizi mazuri kuwa imara kwa mechi zetu zijazo hilo lipo wazi na wachezaji wanalitambua hilo.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwani tunaamini kwamba tutafanya vizuri na kazi itakuwa kwenye ushindani kwenye mechi ambazo tutacheza,’.

Previous articleKHALID AUCHO AMEONGEZEWA DOZI YANGA
Next articleAMEPEWA MECHI MBILI NYOTA MPYA YANGA