AMEPEWA MECHI MBILI NYOTA MPYA YANGA

IKIWA ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga,mshambuliaji Joseph amepewa mechi mbili na Kocha Mkuu Miguel Gamondi kwa leng la kuimarisha uwezo wake pamoja na kuongeza muunganiko pamoja na wachezaji wengine ndani ya kikosi hicho ambacho kinapambana kutetea taji lake la ligi. Ipo wazi kwamba msimu wa 2022/23 ni Yanga ilitwaa ubingwa na msimu huu imeweka wazi kuwa inamalengo ya kutwaa taji hilo.