Home Sports TAIFA STARS KUNA MUDA WALIKUWA WANAONA USHINDI HUU HAPA

TAIFA STARS KUNA MUDA WALIKUWA WANAONA USHINDI HUU HAPA

NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ameweka wazi kuwa kuna wakati waliamini wanashinda mchezo wa hàtua ya makundi dhidi ya Zambia.

Ipo wazi kuwa Tanzania ilianza kupata bao kwenye mchezo dhidi ya Zambia mtupiaji alikuwa ni Simon Msuva dakika ya 11.

Mtibuàji ni Patson Daka dakika ya 89 wakati wakiwa pungufu Zambia baada ya nyota wao mmoja kuonyeshwa kadi ya mbili za njano.

Samatta amesema walipambana kwa nguvu kupata ushindi mwisho ikawa ni Zambia 1-1 Tanzania.

“Tulikuwa na nafasi ya kushinda na kuna muda tulikuwa tunaona kwamba tupo katika nafasi ya kushinda na mwisho imekuwa 1-1. Hatuwezi kubadili matokeo tutafanyia kazi makosa mchezo ujao,”.

Msuva amesema watapambana kushinda mchezo ujao dhidi ya DR Congo ambayo ipo nafasi pili na pointi mbili huku Tanzania ikiwa na pointi moja nafasi ya nne kundi F.

Mchezo ujao kwa Stars ni dhidi ya DR Congo unatarajiwa kuchezwa Januari 24.

Previous articleMIKATABA WALIYOPEWA NYOTA WAPYA SIMBA INA VIPENGELE VIGUMU
Next articleBEKI HUYU BADO YUPO SANA YANGA