LEO Januari 21 timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kuwa na kazi ya kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika, (AFCON).
Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza Stars ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Morocco na leo itakuwa ni mchezo wake wa pili wa kundi F.
Hemed Morocco, Kaimu Kocha Mkuu wa Stars amesema: “Vijana wako tayari na wanaitaka mechi, tumejiandaa vizuri na kuna mambo tumerekebisha. Tunaamini tutafanya vizuri,” Hemed Suleiman ‘Morocco”.
“Mechi itakuwa ngumu lakini vijana wako tayari, tutapambana,” Juma Mgunda, kaimu Kocha Msaidizi wa Taifa Stars.