DR CONGO NGOMA NZITO MBELE YA MOROCCO

TIMU ya taifa DR Congo imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Morocco katika mchezo wa Kombe la Mataifa Afrika, Januari 21.

DR Congo ina wachezaji wawili wanaoitambua Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na Fiston Mayele aliyewahi kucheza Yanga na Henock Inonga anayekipiga Simba.

Morroco walipachika bao kupitia kwa Achraf Hakim mapema kabisa dakika ya 8 na lile la DR Congo lilifungwa na Silas Katompa dakika ya 76.

Ngoma ilikuwa nzito kwa wababe hawa ambapo Morocco wanafikisha pointi nne na DR Congo wakiwa na pointi mbili kibindoni.

Mchezo ujao saa 2:00 usiku ni Zambia v Tanzania ikiwa ni kete ya pili kwa Stars.