MBWA ATAFUNA DOLA 4000 ZA MMILIKI WAKE

Cecil, mbwa kutoka Pennsylvania, amekuwa maarufu baada ya kutafuna bahasha ya pesa ambayo wamiliki wake walikuwa wametenga kwa ajili ya kumlipa mkandarasi.

Mapema Desemba, Clayton Law aliweka bahasha iliyokuwa na $4,000 kwenye kabati lake jikoni kwake huko Pittsburgh, Pennsylvania.

Yeye na mke wake, Carrie, walihitaji kumlipa mkandarasi wao pesa taslimu kwa ajili ya kuweka uzio.

Dakika 30 baadaye, kwa mshangao, walimkuta mbwa wao kipenzi akifurahia mlo wa thamani zaidi maishani mwake, akiacha vipande vichafu vya pesa vilivyotawanyika kila mahali.
m
BBCCopyright: BBC

“Ghafla Clayton alifoka kwa sauti, ‘Cecil anakula $4,000!'” Carrie Law alisema katika mahojiano na gazeti la Pittsburgh City Paper. “Nilifikiri, ‘Sijasikia vizuri.’ Nilisogea na kupata mshtuko wa moyo.”

“Yupo tofauti unaweza kuacha nyama kwenye meza, na asiiguse kwa sababu yeye si mpenzi wa chakula,” Carrie Law alisema. “Lakini inaonekana anapenda pesa.”

Wenzi hao walimpigia simu mara moja daktari wa mifugo wa Cecil ili kuona kama angehitaji matibabu yoyote.

Daktari wa mifugo wa Cecil aliwaambia wenzi hao mnyama wao huyo atakuwa sawa.

Kisha wanandoa walianza zoezi ambalo hawakulitarajia na la kuchosha: Kuunganisha pamoja noti zao zilizochanwa.

Kabla hata hawajaanza kuziunganisha, ilibidi wamngoje Cecil kukohoa na kutoa pesa zingine. Baada ya hapo, walisafisha vizuri.

Walifanya kazi kutafuta nambari za noti katika pande zote za pesa ili kuhakikisha benki zinakubalika na kupewa noti mpya kama mbadala.

Benki ilichukua noti nyingi kasoro dola 450 ambazo haikuweza kurejesha.