SIMBA YATAMBULISHA NYOTA WAKE WA KWANZA

RASMI Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa kiungo, Saleh Karabaka kutoka JKU ya Visiwani Zanzibar kwa mkataba wa miaka mitatu.

Karabaka mwenye umri wa miaka 23 anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Simba SC katika dirisha hili dogo la usajili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waajiri wake hao wapya, Karabaka tayari amejiunga na kikosi hicho kwaajili ya michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea kutimua vumbi visiwani humo.

Simba inatarajiwa kutupa kete yake ya kwanza Januari Mosi kwenye Kombe la Mapinduzi itakuwa dhidi ya JKU SC ikiwa ni mchezo wa fungua mwaka 2024.