Home Uncategorized UGOMVI UWEKWE KANDO, LIGI IENDELEE

UGOMVI UWEKWE KANDO, LIGI IENDELEE

USHINDANI ambao unaendelea kwenye Ligi Kuu Bara unazidi kuonyesha namna ukomavu wa soka letu linavyozidi kukua kila iitwapo leo.

Kuna mengi ya kuendelea kuyaboresha ili ligi izidi kuwa imara zaidi. Kwa upande wa wachezaji pamoja na sehemu ambayo inaamua matokeo yenyewe ikiwa ni uwanja.

Ubora wa uwanja ni daraja kubwa kwa kuendeleza kutoa burudani ambapo furaha ya wachezaji ni kuona kwamba wanakuwa kwenye mwendo mzuri wakiwa uwanjani katika kutafuta ushindi.

Ukweli ni kwamba kuna tatizo la viwanja hilo lipo wazi na hata vile vilivyopo vingihavijakidhi vigezo na ndio maana kumekuwa na kesi ya kufungia viwanja ili maboresho yafanyike.

Kuna umuhimu mkubwa kufanyia maboresho sehemu ya kuchezea kwa kuwa hiyo inatoa picha ya maandalizi ambayo yamefanyika kwa muda.

Hakuna mchezaji anayependa kuona anapata maumivu kutokana na kucheza sehemu ambayo si salama kwake hivyo uboreshaji kwenye eneo la kuchezea ni muhimu kufanyika kwa ajili ya matokeo ya kesho.

Muda uliopo kwa sasa ni kuendelea kufanya mipango mizuri kwaajili ya kukamilisha mzunguko wa kwanza ambao ushindani wake ni mkubwa.

Wachezaji wanatambua namna hali ilivyo hivyo kikubwa ambacho kinatakiwa ni kuona kila mmoja anatimiza majukumu yake kwa wakati pale anapopata nafasi.

Mashabiki nao wasiache kujitokeza uwanjani kushuhudia timu zao zikiwa zinacheza kwa kuwa wanaongeza nguvu kwa wachezaji ndani ya dakika 90 kutafuta ushindi muhimu.

Muda uliopo ni sasa kufanyia kazi makosa yaliyopita na hali hii itaongeza ufanisi na ushindani zaidi kwenye kila idara ndani ya timu.

Kila timu mpango kazi wake ni kupata matokeo hivyo kwa wale ambao hawajawa kwenye mwendo mzuri ni muda wa kufanya maboresho kwenye makosa yaliyopita.

Ipo wazi kwamba kila timu inahitaji kupata matokeo mazuri lakini kuna wachezaji wanaokwama kuonyesha viwango vyao katika mechi za ushindani.

Kwenye mapambano ya kusaka ushindi ni muhimu kuongeza nidhamu ndani ya uwanja nan je ya uwanja. Hilo litafanya kazi ziende kwa umakini na benchi la ufundi kupata fursa ya kuwatumia wachezaji wote ambao wapo katika kikosi.

Ikiwa wapo watakaokuwa wanakwenda tofauti kwenye maandalizi ya mechi husika ni muhimu kurejea kwenye njia wakati ujao na kufanya kazi kubwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi zinazofuata.

Kwa zile timu ambazo bado zinatambua mwendo wao haujawa mzuri ni muhimu kuangalia pale ambapo wanakosea ili kupata matokeo mazuri kwa mechi zijazo.

Furaha ya mashabiki inahitajika kwa kuwa wanachohitaji wao ni kuona timu inapata matokeo chanya. Kupatikana kwa matokeo mazuri haitokei kawaidani kwa juhudi isiyokuwa ya kawaida kila wakati.

Jambo la msingi kwa mashabiki ni kuamini kwamba dakika 90 zinabeba maamuzi ya matokeo ya uwajani. Kazi yao moja kubwa iwe katika kushangilia bila kuchoka.

Kufanya kwao hivyo kutaongeza nguvu kwa wachezaji kuendelea kujituma na kutafuta matokeo kwenye mechi ambazo watakuwa wanacheza.

Muda ni sasa kuendeleza furaha kwa kujitokeza uwanjani na kushangilia timu bila kuchoka huku ugomvi ukiwekwa kando.

Merry Christmas.

Previous articleSAKURA WIND SLOTI YA KUFUNGIA MWAKA MERIDIANBET KASINO
Next articleMWAMBA LUSAJO ANASEPA NAMUNGO