YANGA WANA BALAA HAO, AZIZI KI HASHIKIKI

NDANI ya Ligi Kuu Bara Yanga wana balaa kwenye msako wa pointi tatu huku nyota wao Aziz KI akiwa hashikiki kwenye kucheka na nyavu.

Kasi yake imekuwa katika ubora ambapo alitoka kufunga mabao mawili kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar na Desemba 23 alifunga tena bao moja pekee ambalo liliipa pointi tatu muhimu Yanga.

Jumla ana mabao 10 kibindoni akiwa ni namba moja kàtika utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kuwa shuhuda ubao wa Uwanja wa Jamhuri Dodoma ukisoma Tabora United 0-1 Yanga ni Aziz KI alipachika bao hilo dakika ya 21.

Yanga ni namba mbili kwenye msimamo poiñti 30 baada ya kucheza mechi 11 ña vinara ni Azam FC wenye poiñti 31 baada ya kucheza mechi 13.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kila timu iliingia uwanjani ikiwa na hesabu ya kukomba pointi tatu, mwisho Yanga wakaibuka wababe.