SINGIDA FOUNTAIN GATE: USHINDANI NI MKUBWA

KOCHA msaidizi wa  Singida Fountain Gate Thabo Senong ameweka wazi kuwa ushindani ndani ya ligi ni mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji ushindi ndani ya uwanja.

Timu hiyo baada ya kucheza mechi 14 kibindoni ina pointi 20 huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imetupia jumla ya mabao 17.

Desemba 21 ilikuwa siku mbaya kazini kwa timu hiyo baada ya kushuhudia ubao wa Uwanja wa Nyankumbu ukisoma Geita Gold 1-0 Singida Fountain Gate bao likipachikwa na Valentino Mashaka dakika ya 79.

Kocha huyo amesema:”Kwenye kila mechi ambazo tunacheza tunakutana na ushindani mkubwa nah ii inatokana na kila timu tunayokutana nayo kuhitaji pointi tatu kama ambavyo sisi tunahitaji.

“Ambacho tunakifanya ni maandalizi mazuri na wachezaji kuwa tayari kutimiza majukumu yao. Hilo tunawapongeza na tunaamini wataendelea kufanya vizuri kwa mechi zijazo,”.