UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utarejea kwenye wao kwa wakati mwingine ndani ya Ligi Kuu Bara 2023/24 kutokana na mwendo wao kuwa wa kusuasua.
Simba chini ya Kocha Mkuu, Abdelhak Benchkha imeufunga mwaka 2023 kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma KMC 2-2 Simba.
Matokeo hayo yamemuibua Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo Ahmed Ally na kutuma ujumbe kwa mashabiki wao na timu kwa ujumla akiwasihi kutokata tamaa.
“Tutarejea tukiwa imara zaidi. Hatupaswi kukata tamaa nafasi ya kufanya vizuri bado tunayo hatujafika hata nusu ya msimu.
“Matokeo ambayo tumeyapata hayakuwa yale ambayo tulikuwa tunayatarajia lakini ni mpira na tunaamini kwamba kuna maboreshoo yatafanyika ili kuwa bora na tutarejea kwenye ubora wetu,”.