KWENYE usiku wa tuzo Tuzo Desemba 11 mchezaji bora wa mwaka kutoka kwenye mashindano ya vilabu ambaye kasepa na tuzo hiyo ni Percy Tau wa Al Ahly.
Nyota huyo amewashinda wachezaji wenzake ambao alikuwa nao kwenye fainali ambao ni Peter Shalulile wa Mamelodi na Fiston Mayele ambaye yupo ndani ya Pyramids akitokea Yanga.
Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kutoka kwenye mashindano ya vilabu kwa wanawake ni Fatima Tagnaout (Morocco) akiwapiku Refilwe Tholakeke (Botswana) na Lebohang Ramalepe (Afrika Kusini).
Kwa upande wa mchezaji bora kijana upande wa wanaume imekwenda kwa Lamine Camara (Senegal) akiwapiku Amara Diouf (Senegal) na Abdessamad Ezzalzouli (Morocco).
Tuzo ya mchezaji bora kijana kwa wanawake imekwenda kwa Nesryne El Chad (Morocco), akiwapiku Comfort Yeboah (Ghana) na Deborah Abidoun (Nigeria)