DAKIKA 90 zimekamilika Uwanja wa Mkapa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Yanga kutoshana nguvu na Al Ahly.
Ubao umesoma Yanga 1-1 Al Ahly ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi.
Bao la Al Ahly lilifungwa dakika ya 86 kupitia kwe Percy Tau na lile la usawa ni mali ya Pacome Zouzoa dakika ya 90.
Yanga inakuwa na pointi moja kibindoni baada ya kucheza mechi mbili katika hatua ya makundi na Al Ahly wao wanafikisha pointi nne wakiwa nafasi ya kwanza Kundi D.