Home Sports AZAM FC YAFUNGA NOVEMBA KIBABE

AZAM FC YAFUNGA NOVEMBA KIBABE

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamefunga Novemba kibabe kwa kukomba pointi zote tisa walizokuwa wanazisaka katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara.

Kwenye mechi hizo tatu Azam FC mbili ilicheza ugenini ilikuwa Mashujaa 0-3 Azam FC Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, Ihefu 1-3 Azam FC Uwanja wa Highland Estate.

Kigongo cha kukamilisha hesabu ya tatu ndani ya Novemba kilichezwa Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Azam FC 5-0 Mtibwa Sugar ikiwa ni ushindi wa kwanza mkubwa kwa Azam FC msimu wa 2023/24.

Ni mabao 11 Azam FC ilifunga huku ukuta ukiokota bao moja kwenye nyavu ugenini dhidi ya Ihefu, clean sheet ni kwenye mechi mbili ndani ya dakika 270.

Timu hiyo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ambapo safu yake ya ushambuliaji baada ya kucheza mechi 10 imetupia mabao 24 na pointi zao kibindoni ni 22.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hashem Ibwe amesema ushindi wa mechi za ugenini uliwaongezea nguvu na morali wachezaji kupambana bila kuchoka.

Tulipata ushindi ugenini, sio ugenini tu kwenye viwanja vigumu hilo liliwaongezea nguvu wachezaji na bado wanaendelea kupambana,” .

Previous articleWACHEZAJI YANGA WAMEPIGWA MKWARA, MAXI, AZIZ, PACOME
Next articleKAZI KIMATAIFA LEO HAKUNA MWENYE SHUGHULI NDOGO