>

SIMBA NI MWENDO WA FULL PACKAGE

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa umechukua muziki kamili wa benchi la ufundi ambalo litakuwa na kazi ya kuwanoa wachezaji wa timu hiyo

Ipo wazi kuwa Novemba 5 baada ya ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 1-5 Yanga mambo yalibadilika kwenye benchi la ufundi, Roberto Oliveira aliyekuwa kocha mkuu alisitishiwa mkataba wake Novemba 7.

Ni Abdelhak Benchikha ambaye amepewa mikoba yake aliwasili Bongo usiku wa kuamkia Novemba 28 akiwa na watu wake wa kazi wawili.

Ni yeye Benchikha, kocha msaidizi Farid Zemiti na kocha wa viungo Kamal Boudjenane ambao wametambulishwa kuanza majukumu ndani ya kikosi cha Simba.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba amesema tayari wamefanya kikao na benchi la ufundi na kuzungumza nao kuhusu maono ya timu hiyo.

Baada kufika hapo mchana akawa na kikao na bodi ili bodi imueleze mwalimu kuhusu historia, malengo na maono ya Simba. Tunaamini mazuri yanakuja ndani ya Simba na furaha itarejea.

“Kocha Abdelhak Benchikha amekuja na walimu wengine wawili. Kocha msaidizi na kocha wa viungo. Ni makocha ambao wameshafanya kazi kwa muda na mwalimu Benchikha hivyo tumechukua full package.”