Home Sports UKUTA WA SIMBA KUSUKWA UPYA

UKUTA WA SIMBA KUSUKWA UPYA

WAKIWA kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy benchi la ufundi la Simba limeweka wazi kuwa kila idara makosa yake yanafanyiwa kazi.

Miongoni mwa sekta ambazo zinafanyiwa kazi ni pamoja na ile ya ukuta chini ya Che Malone, Kennedy Juma, Shomary Kapombe na Mohamed Hussein unasukwa upya kuwa na mwendo mzuri.

Ikumbukwe kwamba ndani ya ligi ukuta wa Simba katika timu zilizo tatu bora ni namba moja kwa kuruhusu mabao mengi nyavuni ambayo ni 11 baada ya kucheza mechi 8.

Daniel Cadena, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa kila idara inafanyiwa kazi ili kuwa bora kwa mechi za ushindani.

“Kupata matokeo mazuri kunahitaji uimara kwenye kila idara kuanzia ile ya ulinzi na ushambuliaji. Ambacho tunakifanya ni kufanyia kazi makosa katika mechi zilizopita ili kuwa imara.

“Wachezaji wanaelewa kile ambacho kinahitajika hivyo kwenye uwanja wa mazoezi makosa tunayafanyia kazi. Muhimu ni kuona tunakuwa na mwendo mzuri na kupata matokeo chanya,” amesema Cadena.

Kwenye mchezo uliopita Simba ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa Novemba 25 ukisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas.

Previous articleKAZI BADO IPO KWA MASTAA HAWA YANGA NA SIMBA KIMATAIFA
Next articleYANGA HAWANA JAMBO DONGO, WATUPA DONGO SIMBA KIMTINDO KIMATAIFA