Home Sports SIMBA WATOSHANA NGUVU KWA MKAPA

SIMBA WATOSHANA NGUVU KWA MKAPA

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ni mashuhuda wakigawana pointi mojamoja na  wapinzani wao ASEC Mimosas wakiwa nyumbani.

Licha ya kuanza kupachika bao la kuongoza hali haikuwa njema kwa upande wao walitunguliwa pia bao kipindi cha pili na wapinzani wao.

Dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Simba 1-1 ASEC Mimosas mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakigawana poiñti mojamoja.

Walianza Simba kufunga dakika ya 44 kupitia kwa Saido Ntibanzokiza kisha kipindi cha pili Serge Pokou akaweka usawa.

Haijawa wiki nzuri kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa baada ya Yanga kupoteza ugenini pointi tatu leo watani zao wa jadi Simba wamegawana pointi mojamoja.

Previous articleMWAKA 1998 YANGA ALIMALIZA KUNDI BILA USHINDI WA MECHI YEYOTE
Next articleKUMEKUCHA YANGA, VYUMA HIVI HAPA VINAKUJA