MATAJIRI wa Dar, Azam FC hawataki utani
kwenye mechi zao za ligi kwa kuweka wazi
kuwa watendelea kasi yao ileile waliyoanza
nayo kwenye mechi za ugenini.
Ipo wazi kuwa kwenye mechi mbili za ugenini
Azam FC inayonolewa na Yusuph Dabo
ilikomba pointi sita mazima ndani ya dakika
180.
Ilianza kushuhudia ubao wa Uwanja wa Lake
Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma ukisoma
Mashujaa 0-3 Azam FC na kete ya pili ilikuwa
Uwanja wa Highland Estate, Ihefu 1-3 Azam
FC.
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC
amesema kuwa bado hawajapoa wanahitaji kuendelea na kasi hiyo
kwenye mechi zote.
“Bado tupo vizuri na benchi la ufundi linawapa
mbinu wachezaji wetu kwa ajili ya mechi zote
kuona kwamba tunapata ushindi hivyo tutazidi
kupambana zaidi kwa ajili ya kupata pointi tatu.
“Ushindani ni mkubwa hilo tunalitambua nasi
tutaendelea kuleta ushindani kwa kuwa tuna
timu bora yenye wachezaji ambao wanaleta
ushindani mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.