WALIOPO MKIANI MUHIMU KUPAMBANIA KOMBE

MUDA wa kufanya kazi kubwa ya kujitoa kwenye nafasi zile za mwisho wengi hupenda kuita mkiani inatosha kwa kuanza kuleta ushindani wa kweli.

Ipo wazi kwamba kila timu inahitaji kupata matokeo mazuri lakini inakwama kutokana na kukutana na ushindani mkubwa zaidi.

Muda uliopo kwa sasa ni kufanya malipo stahiki kwa muda ili kuwa kwenye ubora unaohitajika. Malipo hayo ni kwa wachezaji kufanya kweli kutimiza majukumu yao uwanjani.

Na inawezekana kuwa kwenye mwendo bora ikiwa makosa yatafanyiwa kazi. Kila mmoja anatambua namna hali ilivyo kwenye msimamo wa ligi na ushindani ulivyo mkubwa.

Wale ambao walikwama kupata matokeo mazuri kwenye mechi zilizopita muda ni sasa kufanya kazi kubwa kupata matokeo kwa mechi zijazo.

Mapumziko haya yatumike kwa faida kwa kila mmoja kufanyia kazi mapungufu yake. Hilo litaongeza ushindani na kila timu kupata matokeo chanya.

Wachezaji kujituma na kufanya kweli kwenye kila mchezo ni muhimu na itaongeza ushindani kwenye kila mechi ambazo zitachezwa.

Iwe hivyo kila wakati kwa kila ligi kutokana na ushindani ulivyo mkubwa na kupata matokeo ni ngumu ni maana halisi ya ligi.

Wale wanaofikiria ligi ni kitu chepesi waache kufikiria hivyo na badaa yake wafanya kazi kwa juhudi kupata kile kilcho bora.