Home Sports MSHINDI WA MILIONI MOJA KUTOKA VIBUNDA SPESHO PARIMATCH NA TIGO PESA LEO

MSHINDI WA MILIONI MOJA KUTOKA VIBUNDA SPESHO PARIMATCH NA TIGO PESA LEO

KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya Parimatch kwa kushirikiana na Mtandao wa Tigo Pesa yawasisitizia wateja wake kuendelea kushiriki katika kampeni yao ya ‘Vibunda Spesho’ ambayo imesalia masaa machache kuchezeshwa kwa droo ya
kumpata mshindi wa milioni moja siku ya leo Ijumaa.

Hayo yamewekwa wazi na Ofisa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa Parimatch Tanzania Bwana Ismael Mohamed wakati alipokuwa akizungumza na Champion mara baada ya kumaliza kukabidhi zawadi za pesa taslimu shilingi elfu hamsini
(TZS 50,000) kwa washindi 10 kutoka katika droo ya kila siku.

Aidha, Ismael amesema hadi sasa wameshatoa jumla ya kiasi cha milioni mbili kwa washindi arobaini (40) kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na visiwani yaani Zanzibar ambao wamepatikana katika droo ya kila siku ya shindano la Vibunda Spesho na Parimatch.

“Vibunda Spesho bado inaendelea na jambo zuri ni kwamba kwa yoyote atakayekuwa anaweka pesa na tigo na kubashiri na Parimatch anakuwa amejiweka katika nafasi nzuri ya kuingia katika droo ya kila siku na hatimaye anaweza kuibuka na kibunda cha elfu 50 papo hapo. Kila siku washindi wanazidi kuburudika kwa kupata Vibunda Spesho kutoka Parimatch kwa
kushirikiana na mtandao wa Tigopesa. ”, amesema Ismael.

Kwa upande wake, Meneja wa Masoko wa Kampuni hiyo, Bwana Levis Paul amewataka vijana na watanzania kiujumla kuchangamkia fursa hiyo ya kujishindia zawadi za fedha ambazo zinatolewa katika kampeni ya Vibunda Spesho na
Parimatch kwa kushirikiana na mtandao wa Tigopesa.

“Niwasii vijana wenzangu waendelee kubashiri na Parimatch huku kwetu kuna mambo mengi mazuri tumewaandalia kwaajili yao. Wateja wa Parimatch na wadau kiujumla niwaombe wakae karibu nasi kwani kuna kubwa kuliko linakuja”, amesema Levis.

Kampeni ya Vibunda Spesho ni mahususi ni mahususi kwa wateja wao wote wa Parimatch wanaotumia mtandao wa Tigopesa na wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga katika kipindi hichi cha kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Aidha, lengo kampeni hiyo ni kuwawezesha wateja wao kuendelea kucheza na kufurahia burudani kabambe kutoka kwako katika kipindi hichi ambacho tunaelekea katika sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya ukaribisho ya 125% hadi kufikia TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao! Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na michezo ya virtual.

Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.

Previous articleSIMBA YAGAWANA POINTI NA NAMUNGO NYUMBANI
Next articleHUU WAKATI SAHIHI MASHABIKI SIMBA WAAMUE KUWA DAWA AU SUMU