MKWANJA MREFU ATAKUJA TEN HAG

INAELEZWA kuwa ikiwa Klabu ya Manchester United itaamua kuvunja mkataba na kocha Erik Ten Hag italazimika kumlipa zaidi ya pauni milioni 15.

Ten Hag ambaye huu ni msimu wake wa pili ndani ya kikosi hicho anaonekana kuwa na wakati mgumu kutokana na matokeo yanayopatikana kutoridhisha.

Kuna vuguvugu la Ten Hag kuvunjiwa mkataba wake kikosini hapo huku kocha wa Sporting Lisbon, Ruben Amorim na Zinedine Zidane wanatajwa kuwa warithi wake.

Alitambulishwa Man United Julai Mosi 2022 mkataba wake unatarajiwa kugota mwisho Juni 30 2025 ni dili la miaka miwili limebaki mkataba wake kufika tamati.