SIMBA WATOA TAMKO BAADA YA KUPIGWA 5 G NA YANGA

NGOMA imekamilika kwa Simba kupoteza mchezo wa Kariakoo Dabi ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga.

Mabao ya Aziz KI, Max Nzengeli ambaye alifunga mawili, Pacome kwa mkwaju wa penalti na Musonda Kennedy aliyefungulia pazia la mabao dakika ya tatu yametosha kuwatuliza Simba.

Bao pekee la Simba lilifungwa na Kibu Dennis ambaye alitumia pasi ya Saido Ntibanzokiza.Baada ya Simba kunyooshwa mabao hayo matano na watani wa jadi.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram:”Tumezidiwa na mpinzani wetu na hatimae tumeadhibiwa, hakuna unachoweza kusema zaidi kukiri udhaifu kwa upande wetu.Hili limepita japo linaumiza na haliwezi kufutika katika mioyo yetu lakini muhimu ni kuganga yajayo

Tusipoteze focus, mbele yetu tuna mechi nyingi za kupigania malengo yetu

Tumepoteza mechi moja bado tuna mechi nyingine mbele za kupigania malengo yetu.