Home Sports WYDAD HAO FAINALI AFL

WYDAD HAO FAINALI AFL

KLABU ya  Waydad Casablanca ya Morocco  imefanikiwa kutinga hatua ya Fainal katika Mashindano ya African Football League mara baada ya kuiondosha Klabu ya Esperance De Tunis kwa Mikwaju ya Penati

Klabu ya Wydad Imeibuka ushindi wa magoli 5 yaliyopatikana kwenye mikwaju ya Penati dhidi ya Esperance walioapata magoli 4 katika mikwaju ya Penati

Watakutana na miamba kutoka Afrika Kusini dhidi ya Mamelod Sundowns iliyopenya dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Ikumbukwe kwamba Mamelod walipata ushindi wa bao 1-0 kwenye nusu fainali ya kwanza katikamchezo uliochezwa Afrika Kusini bao ambalo walilinda mpaka mwisho wa mchezo.

Timu ambazo zilifungua mashindano hayo zote zimeondolewa kwenye mashindano hayo mapya ambayo yanakwenda kuhitimishwa kwa kumpata bingwa wa kwanza kati ya wababe hawa wawili.

Previous articleMANCHESTER UNITED YAMEWAKUTA TENA
Next articleBEKI WA KAZI YANGA AWAITA MASHABIKI KWA MKAPA