Home Sports HIKI NDICHO ANACHOFIKIRIA NZENGELI WA YANGA

HIKI NDICHO ANACHOFIKIRIA NZENGELI WA YANGA

MAXI Nzengeli kiungo wa Yanga amesema furaha yake kubwa kufunga ni kwa ajili ya mashabiki.

Kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Singida Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa Mkapa alitupia mabao mawili yaliyoipa pointi tatu Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi.

Mchezo unaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa Novemba 5 2023 ikiwa ni Kariakoo Dabi.

Nyota huyo ndani ya Ligi Kuu Bara katupia mabao matano kibindoni akiwa ni namba tatu kwa nyota wenye mabao mengi ndani ya ligi.

“Ninapenda kuona mashabiki wanafurahi na kufunga hilo ni jambo ambalo huwa ninaomba itokee. Kikubwa ni pointi tatu ambazo tunazipata kwenye mchezo husika,”.

Previous articleBARCELONA YAPASUKA EL CLASICO
Next articleHAPA NDIPO TATIZO LA SIMBA LILIPO