KAGERA YAIPIGIA HESABU KALI DODOMA JIJI
UONGOZI wa Kagera Sugar umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi kuu Bara unatarajiwa kupigwa Oktoba 25, kwenye Dimba la Jamhuri mjini Dodoma. Ofisa Habari wa Kagera Sugar, Hamisi Mazanzala aliliambia Championi Jumatano kuwa, maandalizi yapo sawa kwa ajili ya mchezo huo. “Maandalizi yapo sawa na wachezaji wapo tayari kupambana…